Uncategorized

SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU MOLINGA, YAICHOKONOA YANGA KIMTINDO

admin June 12, 2020 11:47 am


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa Yanga wanamkosea David Moliga kwa kumzungushazungusha licha ya kwamba ni mchezaji mzuri ndani ya timu hiyo.

Juni 10, kikosi cha Yanga kilianza safari kuelekea Shinyanga kuifuata Mwadui FC ambapo mchezo wao wa ligi utachezwa kesho Uwanja wa Kambarage.

Kwenye msafara wa kwanza, David Molinga hakuwepo kwa kile ambacho alieleza kuwa hajajumuishwa kwenye kikosi.Jambo hilo lilipingwa na Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli ambaye alisema kuwa Molinga alibaki mwenyewe kwa sababu binafsi.

Manara amesema:”Unajua naona bado kuna mambo ambayo hayapo sawa, haiwezekani mchezaji mzuri anakuwa anapata tabu namna hii, mara aachwe mara inakuaje sasa unamtesa mchezaji mwenye uwezo tena anaongoza kwa kufunga?

“Ni aibu kwa klabu ya Yanga mchezaji kuzunguka kwenye vyombo vya habari akizungumza migogoro yake, hii ni mbaya na haileti picha nzuri,” amesema.

Leo Molinga mwenye mabao nane amekwea pipa akiwa pamoja na Kocha Mkuu, Luc Eymael kujiunga na timu ambayo itacheza Juni 14.

BERNARD MORRISON AONGEZA IDADI YA WATAKAOUKOSA MCHEZO WA MWADUI FC AZAM FC KUSHIRIKIANA NA TFF MAADHIMISHO YA SIKU YA UTOAJI DAMU DUNIANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply