Uncategorized

SIMBA YAPANIA KUIBUKA NA USHINDI MBELE YA MWADUI FC

admin June 16, 2020 10:47 am

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mechi zote zilizobaki ikiwa ni pamoja na ile ya Mwadui FC itakayopigwa Juni 20, Uwanja wa Taifa.

Simba itaingia kwenye mchezo huu ikiwa na roho ya kisasi baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kambarage,Oktoba 30 kutunguliwa bao 1-0.
Sven amesema:”Nafikiri tuna kazi kubwa kwenye mechi zetu zote zilizobaki, hatutatazama tunacheza na timu iliyo nafasi ipi sisi tuna kazi ya kutafuta ushindi kwa namna yoyote.
β€œKwa nanmna ambavyo ligi itakuwa naona kutakuwa na ushindani mkubwa uwanjani ila hilo halitupi presha lazima tupambane kupata matokeo,” alisema. 

Juni 14, Simba ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Ruvu Shooting huku Mwadui FC ikiwa imetoka kuchapwa bao 1-0 mbele ya Yanga, Juni 13.
WINGA WA CONGO ATAJA SIKU YA KUTUA YANGA BERNARD MORRISON BADO PASUA KICHWA YANGA, KESHO KUIKOSA JKT TANZANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply