Uncategorized

SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA MWADUI FC

admin June 18, 2020 9:47 am
SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mechi zote zilizobaki ikiwa ni pamoja na ile ya Mwadui FC itakayopigwa Juni 20, Uwanja wa Taifa.
Simba itaingia kwenye mchezo huu ikiwa na roho ya kisasi baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kambarage,Oktoba 30 kutunguliwa bao 1-0.
Sven amesema:”Tuna kazi kubwa kwenye mechi zetu zote zilizobaki, hatutatazama tunacheza na timu iliyo nafasi ipi sisi tuna kazi ya kutafuta ushindi kwa namna yoyote.
β€œMchezo wetu uliopita tulipata sare ya kufungana bao 1-1 na Ruvu Shooting ipo wazi, lakini ni lazima tuyafanyie kazi makosa yetu ili kupata matokeo mazuri,” amesema.
BUSUNGU AFUNGUKIA USAJILI WAKE YANGA HAWA NDIO SINGIDA UNITED, MWANA KULITAKA, MWANA KULITAFUTA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply