Uncategorized

KUMUONA BERNARD MORRISON NI BUKU TANO TU

admin June 23, 2020 9:47 pm


LEO saa moja kamili Usiku, Uwanja wa Taifa kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Namungo FC. 

Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni mzunguko wa pili unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael mkali wao wa kucheka na nyavu ni David Molinga akiwa na mabao nane huku kwa Namungo mtupiaji wao namba moja ni Relliants Lusajo mwenye mabao 12.

Kuwaona nyota wa Yanga wakimenyana na Namungo, ikiwa ni pamoja na Bernard Morrison mwenye mabao matatu huku kwa Namungo akiwa ni Lukas Kikoti mwenye mabao manne kiingilio cha chini kabisa ni buku tano (5,000) kwa viti vya mzunguko.

 VIP A 15,000 , B&C 10,000 na mzunguko 5,000 huku kwa yule atakayenunua jezi ya Yanga kwa shilingi 20,000 atapewa tiketi bure ya mzunguko na jarida pia.


JEMBE LINALOTUA SIMBA NI NOMA, YANGA WALISHINDWANA NAYE KWENYE MKWANJA LIVERPOOL IMEBEBA MATUMAINI KIBAO KUTAWALA SOKA LA ENGLAND

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply