Uncategorized

SIMBA YASHINDWA NA NYOTA SHONGA KWENYE DAU, SASA KUTIMIKIA URENO

admin June 26, 2020 9:47 am


JUSTIN Shonga, mshambuliaji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini inaelezwa kuwa yupo mbioni kujiunga na Klabu ya CS Maritimo ya nchini Ureno, hiyo ni baada ya kushindwana na Simba.
Shonga raia wa Zambia, inaonekana ameshindwana na klabu hiyo kwa kuwa dau lake la usajili lipo juu sana. Inatajwa thamani yake sokoni ni euro 600,000 (zaidi ya Sh bilioni moja), sasa huenda hiyo ilikuwa kikwazo kikubwa kwa Simba ambayo ilikuwa imeshakubali kumlipa mshahara wa Sh mil 34 kwa mwezi, kwa mujibu wa watu wake wa karibu.
Taarifa za uhakika kutoka kwa mtu wa karibu wa mshambuliaji huyo anayeishi Afrika Kusini, zinasema kuwa mshambuliaji huyo anajipanga kuelekea barani Ulaya baada ya kupata timu hiyo kutokana na kugomea ofa za klabu za Afrika alizokuwa akipokea.
Chanzo hicho kilisema kuwa Mzambia huyo anatarajia kutimkia kwenye nchi hiyo baada ya mazungumzo yake na klabu ya CS Maritimo ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Ureno kuwa katika hali nzuri.

β€œShonga amefanya maamuzi ya kubadilisha upepo kwa sababu ameamua kwenda kucheza Ulaya na atakwenda nchini Ureno kujiunga na Klabu ya CS Maritimo kwa sababu timu nyingi za Afrika zimeshindwa kufikia muafaka naye.
β€œSasa hivi kumekuwa na mazungumzo na Orlando kwa kuwa bado wao ndio wanammiliki kwa sababu ya mkataba wake lakini kwa upande wa mchezaji ameonyesha utayari kwa kwenda kucheza Ureno na siyo kuendelea kucheza Afrika,” kilisema chanzo.
HASSAN KESSY – BILA MILIONI 80 SIJI YANGA..!! MAJEMBE MANNE YA KAZI YAANDALIWA KUZIBA PENGO LA LAMINE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply