Uncategorized

SIMBA YATAJA SABABU YA KUSHINDA LEO MBELE YA NDANDA FC

admin July 5, 2020 11:47 am

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wana sababu zaidi ya tano zitakazowafanya washinde mechi zao zilizobaki ikiwa ni pamoja na ya leo dhidi ya Ndanda.
Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara wana kazi ya kucheza mechi mbili nyanda za juu kusini ambapo ya kwanza itakuwa dhidi ya Ndanda FC, Uwanja wa Nangwanda Sijaona na ya pili itakuwa Julai 8, Uwanja wa Majaliwa dhidi ya Namungo FC.
Akizungumza na Spoti Xtra Sven alisema kuwa sababu kubwa ambazo zinamfanya aamini kwamba atapata ushindi kwenye mechi zake ni pamoja na upana wa kikosi alichonacho jambo linalompa fursa kuamua aanze na nani.
β€œNina wachezaji wengi ambao wana ubora mkubwa, hao wananipa sababu ya kuamini ninaweza kushinda, uwezo wa kila mchezaji kuamua kutafuta matokeo ndani ya uwanja pamoja na ushirikiano ambao upo ndani ya timu.
β€œPia baada ya kuwa mabingwa tumetimiza lengo la kwanza hivyo tutacheza bila presha kubwa uwanjani kwa kuwa hatuna cha kupoteza zaidi ya kutoa burudani na mwisho kabisa ni kwamba tunahitaji ushindi ndio maana tunaingia uwanjani,” alisema.
Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 79 baada ya kucheza mechi 32 za ligi inakutana leo na Ndanda iliyo nafasi ya 17 na pointi 35 zote zimecheza mechi 32.
YANGA YAPIGA HESABU KUWEKA REKODI MPYA KARUME LEO DAVID MOLINGA AIPIGA MKWARA BIASHARA UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply