Uncategorized

BIASHARA UNITED KESHO WANA JAMBO LAO PALE KARUME MBELE YA RUVU SHOOTING

admin July 7, 2020 6:47 pm

FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa  Biashara United amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kusaka ushindi mbele ya Ruvu Shooting. 

Mchezo huo utachezwa kesho Uwanja wa Karume ambapo akishinda ama kulazimisha sare atafikisha jumla ya mechi 10 bila kufungwa Uwanja wa Karume.

Mchezo wake uliopita ililazimisha sare ya bila kufungana na Yanga ndani ya dakika 90, Julai 5 huku Ruvu Shooting nao wakitoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar,  Uwanja wa Kaitaba.

Baraza amesema:”Tupo tayari kupata matokeo mbele ya Ruvu Shooting tunawaheshimu wapinzani wetu ila tutakuwa nyumbani na mashabiki wetu pia.

“Rekodi ya kufikisha mechi 10 bila kufungwa ni jambo jema na imani yangu baada ya dakika 90 tutajua tupo wapi na tumefanya nini mashabiki wajitokeze kutupa sapoti, ” amesema.

MASHINE YA KAZI YANGA YATUA LEO BUKOBA NA KUTINGA MAZOEZINI, KESHO KUVAANA NA KAGERA SUGAR MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply