Uncategorized

MTIBWA SUGAR YATAJA SABABU YA KUIMALIZA AZAM FC GAIRO

admin July 16, 2020 11:47 am

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa sababu kubwa iliyowapa ushindi jana mbele ya Azam FC ni kujituma kwa wachezaji wake ndani ya uwanja muda wote bila kuchoka.


Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba ilikubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuber Katwila.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Gairo, Morogoro ulikuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Mtibwa Sugar inapambana isishuke daraja huku Azam FC ikipambana kupambana kushinda ili kumaliza nafasi ya pili.

Katwila amesema:”Tulipoteza mchezo wetu uliopita mbele ya Mbao FC haina maana kwamba hatukuwa na uwezo hapana, wachezaji wanatambua kazi yao na wameonyesha juhudi mwanzo mwisho hivyo ndio tumeweza kupata ushindi.

“Bado tunapambana kujitoa hapa tulipo kwani mambo mengi yapo na ushindani ni mkubwa ila tunaamini kwamba tutaendelea kupata matokeo.”

Ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 41 huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi 65 zote zikiwa zimecheza mechi 35.

YANGA YAWEKEZA NGUVU ZOTE HUKU BAADA YA KUPOTEZA LIGI KUU BARA NA FA KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA MBAO FC UWANJA WA TAIFA ALLY SALIM NDANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply