Uncategorized

SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA MADAWA KWENYE VYUMBA PAMOJA NA AC

admin July 16, 2020 10:47 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa unashangazwa na taarifa ambazo huwa zinaeleza kuwa timu hiyo huwa inamwaga dawa kwenye mechi zake pamoja na kudaiwa kupulizia dawa kwenye AC jambo ambalo halina ukweli kwani wana kikosi kipana.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa amekuwa akishangazwa na taarifa kuhusu AC pamoja na dawa kitu ambacho huwa hawafanyi.

“Unajua ukitoka nje utaskia sijui AC mara madawa yanawekwa duh mpaka anajiuliza hivi hawa watu wanajua upana wa kikosi cha Simba? Kuna watu wanajua kuuchezea mpira ila wanaishia benchi na sio ndani ya uwanja.

“Yupo Sharaf Shiboub yule jamaa kwa udambwiudambwi tu tuache uongo hafai anajua mpaka anapitiliza lakini ndani ya Simba anasugua benchi unadhani akienda Yanga ama Azam FC anaweza kusugua benchi?

“Hakuna kitu kinachoitwa dawa ndani ya Simba bali timu imara ndio maana tumetwaa ubingwa tukiwa na mechi mkononi sisi ni mabingwa na tunacheza kibingwa,” amesema.

MIKEL ARTETA ATAJA SABABU YA KUWATUNGUA MABAO 2-1 MABINGWA LIVERPOOL YANGA YAWEKEZA NGUVU ZOTE HUKU BAADA YA KUPOTEZA LIGI KUU BARA NA FA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply