Uncategorized

SIMBA WAANZA KUIVUTIA KASI POLISI TANZANIA

admin July 24, 2020 6:47 pm


BAADA ya Simba kutia timu Moshi, leo kikosi cha Simba kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania. 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 26 Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Taifa,  Simba ilishinda mabao 2-1 na kusepa na pointi tatu mazima. 

Hakuna timu yenye presha ya kushuka ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 zote zina uhakika wa kubaki ndani ya ligi.

Simba inayoongozwa na Sven Vandenbroeck ipo  nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 84 na imeshakabidhiwa ubingwa.

Polisi Tanzania inayonolewa na Malale Hamsini ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 55 kibindoni zote zimecheza mechi 37.

KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI KOCHA NAMUNGO, YANGA MAMBO SAFI,SIMBA YAFUATA BEKI TP MAZEMBE, NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply