Uncategorized

SIMBA YATUA KWA SARPONG, YAIPOTEZA MAZIMA YANGA

admin July 26, 2020 11:47 am


MICHAEL Sarpong, inaelezwa kuwa aliyekuwa mshambuliaji wa Rayon Sports ya Rwanda, Mghana, Michael Sarpong, amekubali kujiunga na miamba ya soka nchini Bongo, Simba.

Nyota huyo inaelezwa amekubali kujiunga na Klabu ya Simba kwa kandarasi ya miaka miwili baada ya uongozi wa timu hiyo kukamilisha mazungumzo na wakala wake, huku dau lake likitajwa kuwa ni Sh milioni 138.


Sarpong alikuwa anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga ila mwisho wa siku wamepotezwa kutokana na dau la nyota huyo kuwa kubwa.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa masuala ya usajili kwa Yanga kwa sasa mambo bado kwa kuwa wana mchezo mkononi hivyo hawana presha.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Masingisa amesema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumzia masuala ya tetesi.

MWAKALEBELA: MKAPA ALIKUWA MTU WA MICHEZO EYMAEL: SINA LAMINE MORO, KASEKE, MORRISON SIJUI ITAKUAJE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply