Yanga dhidi ya TRA United
Yanga SC

Yanga Yamkaanga Manqoba Mngqithi! Kocha Afunguka Mazito Baada ya Kichapo cha Simba

Vardo October 24, 2026 12:26 pm

Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, amekiri wazi kuwa kikosi chake kilicheza chini ya kiwango katika mchezo uliopita wa Kariakoo Derby dhidi ya watani zao wa jadi, Simba SC, huku akisisitiza kuwa sasa wanajipanga kurekebisha makosa haraka iwezekanavyo kuelekea pambano lao lijalo dhidi ya TRA United.

Yanga inashuka dimbani leo kusaka alama tatu muhimu za Ligi Kuu Tanzania Bara ugenini dhidi ya TRA United katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mkoani Arusha.

Akizungumza kabla ya mchezo huo, Mngqithi alikiri kuwa kiwango kilichoonyeshwa na timu yake kwenye pambano la Derby, lililomalizika kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Simba, haikuwa kile walichokitazamia, hivyo ni lazima wajifunze kutokana na makosa hayo ili kurejea kwenye mstari wa ushindani.

“Tunatambua hatukucheza katika kiwango kilichotarajiwa kwenye pambano la Derby. Ni muhimu kwetu kujifunza kutokana na makosa na kuelekeza nguvu zetu zote katika michezo inayofuata,” alisema Mngqithi.

Kocha huyo amesisitiza kuwa kikosi hicho kinahitaji mabadiliko ya haraka na maboresho makubwa ili kuendelea kuwa tishio katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Aidha, Mngqithi ametoa wito kwa mashabiki na wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuipa sapoti timu yao, akiamini kuwa nguvu ya mashabiki itakuwa chachu kubwa ya kuamsha morali ya wachezaji kurejesha heshima yao.

Yanga inaingia kwenye mchezo wa leo dhidi ya TRA United ikiwa na kiu ya kugeuza ukurasa wa kichapo cha Derby, huku ikipania kurejea kwenye njia ya ushindi na kuendeleza mapambano ya kulisaka taji la ligi kuu msimu huu.

Anuary Jabir Atishaa! Kinara wa Mabao Ligi Kuu Atuma Onyo Kali kwa Simba na Yanga Como FC: Safari ya Kushangaza Kutoka Serie D Hadi Ligi ya Mabingwa