Uncategorized

BEN CHILWELL APIGA HESABU ZA KUSEPA LEICESTER CITY

admin July 29, 2020 6:47 am


BEN Chilwell, beki wa Klabu ya Leicester City inaelezwa kuwa mpango wake kwa sasa ni kusepa ndani ya kikosi hicho na anahitaj kwenda kukipiga ndani ya Chelsea.
Frank Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea anahitaji kuongeza beki ndani ya kikosi chake na anakubali uwezo wa Chilwell hivyo anaweza kumuongeza ndani ya kikosi chake ambacho kinatumia Uwanja wa Stamford Bridge kwenye mechi za nyumbani.
Nyota huyo mwenye miaka 23 ameitumikia timu ya Leicester City tangu akiwa na miaka 12 na mkataba wake unatarajia kuisha mwaka 2024.Msimu wa 2019/20 imemaliza ikiwa nafasi ya tano na pointi 62 kibindoni na kuwafanya wasishiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Matumaini ya nyota huyo kubaki ndani ya kikosi hicho yamefifia kwa sasa kwa kuwa haitashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Manchester City ambayo imejihakikishia nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 Brendan Rodgers, Meneja wa Klabu ya Leicester City amesema kuwa nyota huyo ameonesha nia ya kutaka kuondoka lakini wana matumaini ya kubaki naye ndani ya kikosi hicho.
“Hatupo tayari kumuuza kwa sasa kwani ni mchezaji mzuri ni aina ya wachezaji ambao huwezi kukubali waondoke katika timu,tumemwambia atulie kwanza kwa sasa ili tubaki pamoja kisha mambo mengine yatafuata,” amesema.
HII HAPA RATINA YA PLAYOFF LEO PATAWAKA AUSSEMS WA SIMBA NA THIERY WA NAMUNGO WATAJWA KUINGIA ANGA ZA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply