Uncategorized

NYONI ATIMIZA AHADI YAKE KWA SHABIKI WAKE NAMBA MOJA

admin August 1, 2020 1:47 pm

ERASTO Nyoni nyota wa Simba leo Agosti Mosi ametimiza ahadi kwa shabiki yake Jumanne Ulimwengu ya kumnunulia baiskeli ambayo ataitumia kwenda shule.

Nyoni alitoa ahadi hiyo jana, Julai 31 wakati akimkabidhi zawadi ya jezi mtoto huyo.

Ulimwengu alikuwa amevaa jezi ya Nyoni ikiwa imechorwa jina lake na namba ya Nyoni jambo lililomfanya beki huyo ampe zawadi ya jezi pia aliomba apewe baiskel ili aitumie kwenda shule jambo ambalo Nyoni aliahidi kulitimiza na leo limetimia.

Simba ipo Sumbawanga ikiwa kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC itakayochezwa kesho, Agosti 2, Uwanja wa Nleson Mandela.

SIMBA YAPATA HOFU NA UWANJA, KESHO KUIVAA NAMUNGO FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO NAMUNGO KUIFUATA SIMBA KWA TAHADHARI, UZI WA KESHO WATAMBULISHWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply