Albert Kangwanda Afunguka Siri ya Chama na Musonda Kumleta Yanga SC
Nyota mpya wa mabingwa wa soka Tanzania, Albert Kangwanda, amevunja ukimya na kuweka wazi namna mastaa wenzake kutoka Zambia, Clatous Chama na Kennedy Musonda, walivyohusika kwa kiasi kikubwa kumshawishi kufanya uamuzi wa kujiunga na kikosi cha Yanga SC.
Kangwanda, ambaye tayari ameanza kuwasha moto ndani ya kikosi hicho ikiwemo kufunga bao muhimu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi Simba SC visiwani Zanzibar, amebainisha kuwa hakuingia Jangwani kubahatisha, bali alifanya utafiti wa kina kabla ya kusaini mkataba.
Mawasiliano ya Siri Kabla ya Kutua Jangwani
Akizungumza na Mwanaspoti, Albert Kangwanda Yanga imekuwa sehemu ya ndoto zake mara tu ofa ilipofika mezani, na hatua ya kwanza aliyoichukua ni kuwatafuta Wazambia wenzake waliomtangulia klabuni hapo ili kupata picha halisi ya mazingira ya klabu.
“Mara baada ya kupata nafasi ya kujiunga na Yanga, sikusita kufanya mawasiliano na Wazambia wenzangu (Chama na Musonda) ili kufahamu zaidi kuhusu timu hii, utamaduni wake na mazingira yake kwa ujumla,” amesema Kangwanda.
Ushindani wa Namba na Kiu ya Mafanikio
Mshambuliaji huyo ameongeza kuwa ubora wa kikosi cha Yanga na ushindani uliopo ni miongoni mwa sababu zilizomvutia zaidi, akiamini kuwa ni jukwaa sahihi la kukuza kipaji chake na kupiga hatua kubwa kisoka.
Akizungumzia nafasi ya Chama na Musonda ndani ya klabu hiyo, Kangwanda alikiri kuwa kila mmoja aliacha alama yake kulingana na majukumu yake uwanjani, na sasa ni zamu yake kuandika historia mpya.
-
“Wote wawili walifanya sehemu yao na kutekeleza majukumu yao. Ni wachezaji tofauti; mmoja ni mshambuliaji na mwingine ni winga ambaye pia anaweza kucheza namba 10,” alifafanua.
-
“Wote waliipa klabu mchango wao mkubwa, hivyo ninachotakiwa mimi ni kuanzia walipoishia na kuacha alama yangu.”
Maisha Mapya Tanzania na Takwimu Zake Msimu Huu
Mbali na mipango yake ya uwanjani, Kangwanda ambaye hadi sasa ameshahusika kwenye mabao matatu katika Ligi Kuu Bara msimu huu (akifunga mabao mawili na kutoa asisti moja), amesema amepokelewa kwa upendo mkubwa na mashabiki pamoja na wachezaji wenzake, hali inayomfanya ajisikie kama yupo nyumbani Zambia.