Uncategorized

YANGA WAACHANA NA JUMA ABDUL

admin August 5, 2020 5:47 pm


JUMA Abdul, leo Agosti 5 ameachana na timu yake ya Yanga baada ya kushindwa kufikia makubaliano kwenye suala la mkataba wake.

Abdul ndani ya Yanga alikuwa ni nahodha msaidizi na kwa msimu wa 2019/20 amehusika kwenye jumla ya  mabao 6 kati ya 45 yaliyofungwa na Yanga akiwa ametoa pasi sita zilizoleta mabao.

Abdul amesema kuwa wameshindwa kuelewana na mabosi zake wa Yanga hasa kwa upande wa makubaliano ya mkataba wake.

“Tumeshindwa kufikiana makubaliano na Yanga kwenye upande wa mkataba wangu kwa kuwa walitaka kunipa mkataba bila ya kunilipa fedha za usajili hivyo nimeamua kuanza maisha mengine,” amesema.

Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 38 ndani ya LigiKuuBara, Abdul alianza kikosi cha kwanza kwenye mechi 28.

ISHU YA TSHISHIMBI IMEKUJA KIVINGINE,SIMBA YAFANYA UMAFIA,KESHO NDANI YA SPOTI XTRA NAMUNGO FC NAO WAMALIZANA NA JEMBE LA KAZI KUTOKA LIPULI ASAINI MIAKA MIWILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply