Uncategorized

SAINI YA SUREBOY YANGA BADO NI PASUA KICHWA

admin August 6, 2020 12:47 pm

UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa nyota wao Salum Abubakar maarufu kama Sureboy awali hakuwa tayari kuibukia ndani ya Yanga jambo ambalo limesababisha abaki ndani ya timu hiyo mpaka sasa hivyo ikiwa atakuwa amebadili nia hawana hiyana ya kumzuia.


Imekuwa ikiripotiwa kuwa Yanga wapo kwenye hesabu za kuinasa saini ya kiungo huyo mzawa huku taarifa zikieleza kuwa tayari wameshapeleka ofa ili kuipata saini ya kiungo huyo.

Kwa kauli hiyo bado kupatikana kwa saini ya Sureboy Jangwani inakuwa pasua kichwa kwa kuwa Azam FC inaonekana bado wanahitaji huduma ya kiungo huyo.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa waliwahi kumuuliza Sureboy awali hakuwa tayari kuondoka kwa kile alichoeleza kuwa anafurahia maisha ndani ya kikosi.

“Tuliwahi kumuuliza mchezaji kama anaweza kuondoka ndani ya Azam FC alisema kuwa anafurahia maisha ya hapa na kwetu ni mchezaji muhimu ambaye tunamhitaji.

“Ili mchezaji aondoke ni lazima mambo yote yaende kwa usawa ikiwa ni pamoja na mchezaji mwenyewe anataka nini je na timu inahitaji kumuuza?  Hakuna ambaye amesema mchezaji yupo sokoni kwa sasa.

“Hivyo ikiwa yeye atahitaji kuondoka hilo ni jambo jingine na uongozi ukiwa unamhitaji zaidi nalo ni jambo jingine ndio maisha ya soka yalivyo, hakuna ofa ambayo tumepokea kwa sasa zaidi ya kuskia tetesi lakini Sureboy ni Icon wa Azam FC,” amesema.

PACHA WA MWAMNYETO, AME, PICHA ZIMA KUIBUKIA SIMBA LIMECHEZWA HIVI KOSI LAMILI YA YANGA KWA SASA LIPO NAMNA HIO,MASHINE MPYA TANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply