Uncategorized

KOCHA LIPULI ABWAGA MANYANGA

admin August 9, 2020 9:47 am

BAADA ya kushuhudia Lipuli ikishuka daraja kwa msimu wa 2019/20, Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Nzeyimana Mailo ameamua kuachana na kikosi hicho jumlajumla.


Lipuli ya Iringa imemaliza ligi ikiwa nafasi ya 18 ikiwa na pointi 44 kibindoni msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Mailo alisaini dili la miaka miwili kukinoa kikosi hicho amesema:”Changamoto zilikuwa nyingi ndani ya timu ikiwa ni pamoja na suala la malipo ya mishahara kwa wachezaji na madai yao mbalimbali ndani ya timu.

“Niliwasiliana na uongozi ili kusitisha mkataba wangu kabla ya ligi kuisha ila waliniomba nimalize kwanza ligi hivyo baada ya msimu kuisha tumekubaliana kuvunja mkataba na kwa sasa nipo huru,” amesema,

Chanzo:Spoti Xtra
NYOTA WA HISPANIA ANAYETAJWA KUIBUKIA YANGA AFUNGIKIA DILI LAKE PIRLO ARITHI MIKOBA YA SARRI KWA MIAKA MIWILI JUVENTUS

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply