Uncategorized

MTUPIAJI NAMBA MOJA NAMUNGO AWAAGA MASHABIKI WAKE

admin August 10, 2020 3:47 pm

RELIANTS Lusajo mshambuliaji namba moja ndani ya Klabu ya Namungo FC kwa msimu wa 2019/20 leo amewaaga mashabiki na viongozi wake wa Namungo.


Lusajo amefunga jumla ya mabao 12 ndani ya Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery mkataba wake umeisha ndani ya kikosi hicho na hajaongeza dili jingine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lusajo ameandika:”Cha kwanza napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uzima mpaka siku ya leo pili ningependa kutoa shukran zangu za dhati kwa  uongozi pamoja na wachezaji wa Namungo kwa ujumla kwa muda wote tulioishi pamoja.

“Ushirikiano mlionipa tangu kujiunga na timu Daraja la Kwanza mpaka hapa tulipofika,bila kusahau mashabiki wote wa Ruangwa waliokua wakitupa hamasa na support iliyotuwezesha kufikia malengo ya klabu. Nawatakia kila la kheri Mungu awabariki katika msimu ujao,”.

Kuhusu atakapokuwa msimu ujao, Lusajo amesema kuwa itajulikana hivi karibuni.

FUKUTO LA CHAMA KUSEPA SIMBA, UONGOZI WAFUNGUKA ISHU YA MORRISON MAAMUZI BADO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply