Uncategorized

SERIKALI YAIPA TANO AZAM FC

admin August 24, 2020 6:47 am

 


WAZIRI wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Harisson Mwakyembe amesema kuwa Klabu ya Azam FC imeongeza thamani ya soka nchini na kujitengenezea nafasi ya kuwa timu kubwa na bora nchini.


Maneno hayo aliyasema jana Agosti 23, kwenye kilele cha Azam Festival makao makuu ya Azam FC, Chamazi.


Mwakyembe alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa na udhuru.

“Serikali ambapo huwa inakwama kwenye masuala ya kimichezo ikiwa ni pamoja na uwanja huwa inakimbilia huku kwa Azam kwa kuwa mmejipambanua na kuwa bora katika miundombinu pamoja na kuwa na timu bora.


“Pia ni timu ambayo ina academy yake pamoja na miundombinu bora, kwa tamasha ambalo mmelifanya limeongeza thamani ya timu yenu na ninaamini kuwa mtazidi kuwa bora,” amesema.


Burudani zilitolewa kwa mashabiki jana ikiwa ni pamoja na mechi za utangulizi, show kali kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba pamoja na msanii wa Singeli, Msaga Sumu.


BAYERN MUNICH MABINGWA LIGI YA ULAYA, NEYMAR AMWAGA MACHOZI ISHU YA KONDE BOY NA WAWA KUREJEA SIMBA IPO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply