Uncategorized

NAMUNGO KUKUTANA NA MUZIKI WA NYOTA HAWA WA KAZI SIMBA

admin August 27, 2020 7:47 pm


NYOTA wawili wa Klabu ya Simba, Luis
 Miquissone ambaye ni kiungo mshambuliaji na Pascal Wawa ambaye ni beki wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo FC utakaopigwa Agosti 30.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6.

Nyota wote wawili ni watu wa kazi kwa kuwa walikuwa ni chaguo la kwanza kwa Sven Vandenbroeck ndani ya Simba kwenye mechi za ushindani.

Luis raia wa Msumbiji na Wawa raia wa Ivory Coast hawakuwa sehemu ya kikosi kilichotambulishwa Agosti 22, Uwanja wa Mkapa, siku ya Simba day kwa kuwa walikuwa wamepewa ruhusa ambapo walikuwa nchini kwao kwa ajili ya kukamilisha masuala ya ndoa.

Tayari leo wote wamerejea nchini hivyo wanaungana na wachezaji wenzao ambao walikuwa wameshaanza mazoezi kuendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii pamoja na mechi za ligi.


Sven, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kurejea kwa nyota wake ndani ya Simba kunamfanya awe na kikosi kamili kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya mechi zake zote zilizo mbele yake.

NAMUNGO WANA JAMBO LAO KWA WANA ARUSHA, KUTAMBULISHA MAJEMBE MAPYA MATATU MESSI ANUKIA KUTUA MANCHESTER CITY

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply