Uncategorized

YANGA YATOA SHUKRANI KWA MASHABIKI WAKE

admin September 7, 2020 12:47 pm


 UONGOZI wa Yanga umewashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.


Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa na Yanga iligawana pointi mojamoja.


Bao la kwa Tanzania Prisons lilipachikwa kimiani na Lambart Sabiyanka na lile la kusawazishwa kwa Yanga lilipachikwa na Michael Sarpong.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio  Nugaz amesema kuwa mashabiki wanahitaji pongezi kwa kujitoa kuipa sapoti timu yao uwanja wa Mkapa.


“Mashabiki wengi walijitokeza katika hilo tunapenda kuwashuru na kusema asante kwa kujitokeza, ni mwanzo mzuri na imani yetu ni kwamba tutaendelea kujitokeza kwa wingi,” amesema. 

SIMBA YATIA TIMU BONGO, KUANZA KUIPIGIA HESABU MTIBWA SUGAR DODOMA FC NI NOMA, WAWEKA REKODI YAO BONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply