Uncategorized

DODOMA FC NI NOMA, WAWEKA REKODI YAO BONGO

admin September 7, 2020 1:47 pm

DODOMA Jiji FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata jana Septemba 6 iliweka rekodi yake ya kipekee kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya  Mwadui FC.


Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulichezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na iliwalazimu wasubiri mpaka dakika ya 68 kupachika bao la ushindi kupitia kwa nyota wao Khamis Mcha.

Ushindi huo unaifanya iwe timu ya kwanza kushinda kwa timu ambazo zimepanda kwa msimu wa 2020/21.


Gwambina FC ilifungua pazia lake kwa kunyooshwa bao 1-0 mbele ya Biashara United, Ihefu FC ilifungua ligi kwa kufungwa mabao 2-1.  


YANGA YATOA SHUKRANI KWA MASHABIKI WAKE HII HAPA CV YA CEO MPYA WA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply