Dickson Job na Clement Mzize
Yanga SC

Yanga Yachukua Hatua Nzito kwa Job na Mzize: Kupelekwa Afrika Kusini Kwa Vipimo Zaidi

Vardo September 2, 2026 8:08 pm

Klabu ya Yanga imeamua kuchukua tahadhari kubwa ili kuhakikisha mabeki na washambuliaji wake tegemeo, Dickson Job pamoja na Clement Mzize, wanarejea uwanjani wakiwa timamu kwa asilimia mia moja.

Wachezaji hao wawili wamekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu wakipatiwa matibabu na kufuata programu maalum za kurejea mchezoni baada ya kusumbuliwa na majeraha ya goti yaliyowakosesha sehemu kubwa ya msimu uliopita. Kama sehemu ya hatua za mwisho kabla ya kuwarejesha kikosini, uongozi unapanga kuwapeleka nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo maalum vya kimatibabu.

Chanzo kutoka kitengo cha tiba cha Yanga kimeeleza kuwa vipimo hivyo vya mwisho nchini Afrika Kusini vinalenga kuwapa madaktari picha kamili na ushahidi wa kitiba kwamba majeraha ya wachezaji hao yamepona kikamilifu na miili yao ipo tayari kukabiliana na ushindani mkali wa mechi zijazo.

Benchi la ufundi limesisitiza kuwa halina haraka ya kuwarudisha uwanjani bila kujiridhisha, kwani lengo kuu ni kuwaona wakicheza mfululizo bila hatari ya kujirudia kwa majeraha hayo au kuishia kucheza mechi chache kisha kurejea tena chumba cha matibabu.

Mchambuzi Afichua Sababu Doumbia Kukwama Simba SC