Uncategorized

KOCHA ARSENAL ATAKA KILA MCHEZAJI KUFUNGA

admin September 24, 2020 9:47 am

 


MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amewataka wachezaji wake kumsaidia suala la ufungaji mabao straika wao namba moja, Pierre-Emerick Aubameyang.

Kocha huyo alikiongoza kikosi chake kushinda mbele ya West Ham 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England Jumamosi iliyopita, huku watupiaji wakiwa ni Alexandre Lacazette na Eddie Nketiah.

Arteta amewataka wachezaji wahakikishe kwamba wanamiliki mpira huku kila mmoja akiwa na uwezo wa kufunga ili kuwafanya kurudi kwenye ubora wa kuhesabika kama moja ya timu matata Ligi Kuu England.

“Tunahitaji kushiriki pamoja suala la kufunga mabao.
Nilishawaeleza hilo. Tunahitaji kufunga kama timu iwapo tunataka kuchuana na timu kubwa kwenye ligi. Tukitegemea mchezaji mmoja hatutaweza.

“Hivyo, wote ni lazima wawajibike na hilo litawahusu wachezaji wa nafasi zote ili kuweza kufikia malengo.”

RUVU SHOOTING YAZIPIGIA HESABU POINTI ZA BIASHARA UNITED LUIS SUAREZ MALI YA ATLETICO MADRID

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply