Uncategorized

SVEN AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE KWA KUTUMIA VEMA MIPIRA YA ADHABU

admin September 28, 2020 8:47 am

 


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wanazidi kuimarika na kuwa na uwezo wa kutumia mipira ya adhabu tofauti na ilivyokuwa awali.


Simba ilishinda mabao 3-0 mbele ya Gwambina FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo kwenye mchezo huo, beki Pascal Wawa alifunga bao lake la kwanza akiwa nje ya 18 kwa mpira wa faulo.


Sven amesema:”Wachezaji wanazidi kuimarika kila leo ni jambo zuri na linafurahisha hasa ukizingatia kwamba wameanza kufunga kwa kutumia mipira ya adhabu.


“Wawa amefunga bao moja mbele ya Gwambina kwa faulo, ni mpigaji mzuri na kwetu sisi ni furaha kwani awali ilikuwa ngumu kufunga kwa adhabu, mechi zetu zilizopita tulishindwa na ninaamini hii ni mara ya kwanza.


“Hata Luis Miqussone naye alipiga kona ambayo ilifungwa na Meddie Kagere hivyo kuna maendeleo ambayo yameanza kuonekana ndani ya kikosi kwa sasa tofauti na awali.”


Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi nne, imeshinda tatu na sare moja mbele ya Mtibwa Sugar.

MCHEZO MZIMA WA YANGA KUICHAPA BAO 1-0 MTIBWA SUGAR ULICHEZWA HIVI KOCHA SIMBA APATA DILI LA MIAKA MITATU AFRIKA KUSINI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply