Uncategorized

WAHUNI WAMLIZA MUANGOLA WA YANGA

admin October 5, 2020 11:47 am




KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos, amekutana na wahuni wa mtandaoni ambao wamemliza kwa kumuibia akaunti yake ya Instagram.


Carlinhos ambaye amejiunga na Yanga msimu huu, amekutana na balaa hilo ikiwa ni siku chache baada ya kuanza kuonesha cheche zake ndani ya Ligi Kuu Bara.


Dismas Ten ambaye yupo katika Kitengo cha IT ndani ya Yanga, ameposti taarifa iliyosema: “Mwizi, kibaka jambazi punde tu tunamtia mkononi, lakini kwa sasa unaweza kumfollow huyu mwamba kupitia @officialcarlinhos  sasa hivi ili twende sambamba..! @officialcarlinhos imewekwa ulinzi wa kutosha.”


Ishu za watu mbalimbali kuibiwa akaunti zao mtandaoni imekuwa endelevu ambapo wapo wanaofanikiwa kuzikomboa na wengine kuzipoteza kabisa.

MAKOCHA HAWA WAINGIA KWENYE ORODHA YA KUIBUKIA YANGA KIKOSI CHA TIMU YA POLISI TANZANIA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA KMC, UWANJA WA UHURU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply