Uncategorized

RATIBA YA VPL LEO NI JAMHURI, DODOMA

admin October 16, 2020 7:47 am


LEO Oktoba 16 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo mchezo mmoja utachezwa kwa timu mbili kusakapointi tatu muhimu.

 Dodoma Jiji FC itawakaribisha  Mbeya City Uwanja wa Jamhuri Dodoma saa 10:00.


Dodoma Jiji ipo nafasi ya saba kwenye msimamo baada ya kucheza mechi tano na mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mwadui FC msimu wa 2020/21 ilishinda bao 1-0.


Imekuwa na matokeo chanya Uwanja wa nyumbani jambo linaloongeza ugumu kwa Mbeya City ambayo imekuwa kwenye mwendo wa kusuasua kwa msimu wa 2020/21.


Kwenye msimamo ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi tano za ligi.


DYBALA AINGIA ANGA ZA CHELSEA KAZE ASAINI DILI LA MIAKA MIWILI YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply