Uncategorized

BEKI SIMBA AWEKA REKODI YAKE, MUGALU KAMA KAWAIDA

admin October 18, 2020 5:47 am

BEKI wa Simba, Ibrahim Ame ambaye ni ingizo jipya kwa msimu wa 2020/21 akitokea Klabu ya Coastal Union jana Oktoba 17  ameandika rekodi yake kwa kufunga bao lake la kwanza ndani ya kikosi hicho.


Licha ya kwamba ni beki, kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Mlandege FC ya Zanzibar alipachika bao wakati Simba ikishinda mabao 3-1.


Bao hilo alipachika dakika ya 16 na lilikuwa ni la pili kwa kuwa la kwanza lilifungwa na Chris Mugalu ambaye alipachika mabao mawili kwenye mchezo huo.

Bao la kwanza alipachika dakika ya 8 ya mchezo na bao la pili ambalo lilikuwa ni la tatu alipachika dakika ya 68 na kuwafanya Simba waondoke uwanjani wakiwa washindi.

Mlandege FC walipata bao dakika ya 71 kupitia kwa nyota wao Yahya Haji aliyemtungua Aishi Manula mazima. 

TANZANIA KUANDAA MASHINDANO YA AFCON MAZOEZI YA YANGA SI MCHEZO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply