Uncategorized

ARSENAL YAPINDUA MEZA

admin October 23, 2020 4:47 am

 


ARSENAL imeanza kwa ushindi wa mabao 2-1 ndani ya kundi B kwenye Kwenye mashindano ya Europa League baada ya kupindua meza kibabe wakitokea nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Rapid Wien.


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Allianz Stadion Taxiarchis Fountas alianza kupachika bao la Kwanza kwa Rapid Wien lililopinduliwa na David Luis dakika ya 70.


Bao la pili na la ushindi lilipachikwa na nahodha Pierre Emerick Aubameyang dakika ya 74 na kuifanya Arsenal kusepa na pointi tatu jumlajumla wakiwa ugenini.


Mikel Arteta Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa anafurahi kuona vijana wake wanashinda na kuwataka waongeze juhudi zaidi katika kuboresha viwango vyao.

MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA BAADA YA BIRIANI LA SIMBA KULIWA,NENO LAO HILI HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply