Uncategorized

NYOTA AZAM FC ATIMKIA ISRAEL

admin October 23, 2020 5:47 am

 

KIUNGO Novatus Dismas ameuzwa kwenda Klabu ya Macabi Tel Aviv ya Israel kutoka Klabu ya Azam FC.


Nyota huyo mwenye tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa msimu wa 2019/20 dili lake limejibu baada ya kufanya vizuri majaribio yake.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa majaribio yake timu ya wakubwa alifaulu jambo ambalo limewafanya mabosi wa Macabi Tel Aviv kurudi mezani na kupewa kijana huyo raia wa Tanzania.


“Alifanya vizuri majaribio ya kwanza kwa timu ya vijana na alipokwenda timu ya vijana aliweza kufanya vizuri na alipopata nafasi kwenye timu kubwa aliweza kufanya vizuri pia.


“Tumefikiana makubaliano mazuri na timu hiyo hivyo kwa sasa atakuwa ni mali ya Macabi Tel Aviv hivyo kikubwa ni kuona anaweza kufanya vizuri,” amesema.

DAVID KISSU WA AZAM FC AWEKA REKODI YAKE BONGO WANNE YANGA WAINGIA KWENYE VITA YA KUWANIA TUZO BAADA YA KUSHINDA MBELE YA POLISI TANZANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply