Uncategorized

SIMBA MAJANGA TUPU NYOTA WATANO KIKOSI CHA KWANZA OUT

admin October 23, 2020 11:47 am


KUUMIA kwa beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe jana Oktoba 22 kunafanya jumla ya wachezaji watano wa Simba kuwa majeruhi.


Nyota mwingine ambaye ni majeruhi ni Chris Mugalu, raia wa Congo ambaye alipata maumivu ya nyonga muda mfupi kabla ya timu hiyo kuvaana na Tanzania Prisons.


Wengine ambao ni majeruhi ni pamoja na Meddie Kagere na John Bocco ambao wote ni washambuliaji.


Pia Gerson Fraga, kiungo wa Simba pia naye ni majeruhi ambapo aliumia wakati timu ilipokuwa ikipambana na Biashara United.


Simba ilipoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kwa kuchezewa gwaride na Tanzania Prisons ambao walisepa na pointi tatu jumlajumla Uwanja wa Nelson Mandela.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema kuwa kwa sasa ni ngumu kuzunguzia hali za wachezaji hao wakikamilisha utaratibu watatoa taarifa kupitia vyombo vyao vya habari.

MECHI ZA UWANJA WA MKAPA ZAPELEKWA UHURU MTIBWA SUGAR:TUTAFANYA VIZURI 2020/21

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply