Uncategorized

YANGA YATAJA MITAMBO YA USHINDI DHIDI YA NAMUNGO

admin November 21, 2020 8:47 am

 


CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa viungo wake kwa sasa wameshikilia ushindi kwenye mechi zake zote atakazoingia uwanjani ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Namungo utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, kesho Novemba 22.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaze amesema kuwa wachezaji wake wengi kwa sasa wamekuwa bora jambo ambalo anaamini kuwa watampa matokeo mazuri ndani ya uwanja kwenye mechi zake.

Kaze amemtaja kiungo wake Farid Mussa mwenye pasi mbili za mabao na Carlos Carlinhos mwenye pasi mbili na bao moja kati ya 12 yaliyofungwa na kikosi hicho kwenye mechi 10.

β€œNi mbinu kwenye kila mchezo kusaka pointi tatu na kupata mabao mengi ila tumekuwa tukishindwa kufanya hivyo kwa kuwa wachezaji wangu wengi mbinu yao ni moja ya kutokea pembeni.

β€œNimewaambia viungo wangu wote ikiwa ni pamoja na Fard,(Mussa), Carlinhos (Carlos) kwamba wanatakiwa wabadilishe mbinu, wasitegemee mipira ya kutoka pembeni bali wanatakiwa wawe watulivu na mbinu nyingine ambazo nimewapa siwezi kuziweka wazi,” amesema Kaze. 

BERNARD MORRISON, CHAMA WATUMIWA UJUMBE NA WAGOSI WA KAYA HAALAD AWAFUNIKA SANCHO, ANSU, FODEN

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply