Uncategorized

MKWASA AAHIDI KUTOA BURUDANI MBELE YA YANGA KWA MKAPA

admin December 6, 2020 4:47 pm


 KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amesema kuwa wamejipanga kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Yanga na wanawaheshimu wapinzani wao hivyo hawana mashaka katika kusaka pointi tatu.

 Mkwasa amesema hayo muda mfupi kabla ya timu yake kuingia Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu dhidi ya Yanga.


Mkwasa amesema:”Tunaingia ndani ya uwanja tukijua kwamba tunakutana na vinara wa ligi, hilo lipo wazi lakini nasi pia tumejipanga kuona kwamba tunapata matokeo mazuri.

“Burudani ni kitu ambacho tumekuwa tukikifanya lakini ni katika kusaka matokeo mazuri ndani ya uwanja, tunahitaji pointi tatu nasi tupo tayari.


“Kikubwa mashabiki watupe sapoti na kuona namna gani tunaweza kuwa bora na kuzidi kuendelea kutoa burudani ndani ya uwanja,” amesema.

ISHU YA MABAO KIDUCHU NDANI YA YANGA YAFUNGUKIWA NA KOCHA LIVE: YANGA 1-0 RUVU SHOOTING

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply