Simba vs Orlando Pirates Leo: Steve Barker Atoboa Siri ya Ushindi CAFCL
Baada ya Yanga kupoteza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), macho na matumaini ya Watanzania sasa yanaelekezwa kwa wawakilishi wengine wa nchi, Simba SC, ambao leo wanashuka dimbani wakiwa na jukumu zito la kusaka ushindi na kulinda heshima ya soka la Tanzania.
Wekundu wa Msimbazi watawakaribisha Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika mchezo mkali wa Kundi C utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Simba inaingia uwanjani ikiwa na dhamira moja tu: kuanza kampeni zake kwa kishindo mbele ya mashabiki wake wa nyumbani.
Presha ya Matokeo Baada ya Kichapo cha Yanga
Katika msimu huu wa michuano ya Afrika, Tanzania inawakilishwa na vigogo wawili, Simba na Yanga. Hata hivyo, Yanga ilianza vibaya hatua ya makundi baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya MC Alger ya Algeria katika mchezo uliopigwa jana kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Matokeo hayo yanaongeza uzito na umuhimu kwa Simba vs Orlando Pirates leo kuhakikisha alama tatu zinabaki nyumbani.
Kauli ya Kocha Steve Barker Kuhusu Mchezo wa Leo
Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, amesema kikosi chake kipo tayari kimwili na kiakili kuhakikisha kinaanza hatua hii kwa matokeo chanya, akisisitiza kuwa makosa ya msimu uliopita yamewapa funzo kubwa.
Barker amebainisha kuwa msimu uliopita Simba ilishindwa kupata mwanzo mzuri katika hatua ya makundi, hali iliyowaweka kwenye mazingira magumu ya kufukuzia alama katika michezo iliyofuata.
“Kwa bahati mbaya, msimu uliopita hatukuanza vizuri na ilikuwa vigumu baadaye kufukuzia matokeo. Hivyo, mchezo huu ni muhimu sana kwetu katika muktadha wa hatua ya makundi; tunahitaji kuanza vizuri,” alisema Barker.
Mpango wa Kuikabili Orlando Pirates
Kuhusu ubora wa wapinzani wao kutoka Afrika Kusini, kocha huyo amekiri kuwa wanakutana na timu yenye ushindani mkubwa, lakini anaamini viwango vya timu zote mbili vinalingana. Amesema siri ya ushindi itakuwa ni nidhamu ya mbinu na kutumia vyema nafasi zitakazopatikana.
Barker ameongeza kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake pamoja na malengo ya klabu, akisisitiza kuwa dhamira yao kuu ni kukusanya alama za kutosha kwenye kila mchezo wa kundi hilo ili kujihakikishia tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.