Uncategorized

NEYMAR JR KUCHEZA TENA NA MESSI

admin December 7, 2020 8:47 am


 KOCHA wa Barcelona, Ronald Koeman, anaamini kuwa Barcelona itafanya kitu kuona msimu ujao Lionel 
Messi anacheza tena na Neymar ndani ya Camp Nou. 

Hii ni baada ya hivi karibuni, Neymar kutamka wazi kuwa msimu ujao anataka kucheza tena na Messi ingawa haijaelezwa wapi kama ni PSG au Barcelona.

 

Neymar aliondoka Barcelona mwaka 2017 na kutua PSG. Alicheza na Messi ndani ya Barcelona kuanzia 2013, tangu msimu uliopita, staa huyo amekuwa akihusishwa kurejea viunga vya Camp Nou.


 Nyota Messi mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu ambapo awali naye alikuwa anahitaji kusepa ndani ya kikosi hicho.

 

“Kila mmoja anafahamu suala la Messi, mtu pekee ambaye anayeweza kuamua hatma yake kwa sasa ni yeye mwenyewe.


 “Klabu inapambana kuona inakuwa na wachezaji bora , nataka kuona Messi anacheza hapa na mchezaji bora (Neymar) ndani ya Camp Nou itakuwa vizuri zaidi,” amesema Koeman.

YANGA WAKALI WA MECHI ZA UGENINI MASHABIKI WAMPA FURAHA KLOPP WAKATI AKISHUSHA KICHAPO CHA 4G

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply