Uncategorized

SIMBA QUEENS YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA PRINCESS

admin December 11, 2020 3:47 am


MUSA Mgosi, Kocha Mkuu wa timu ya Simba Queens amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya Dar Dabi ya Ligi ya Wanawake Tanzania, kesho Desemba 12 dhidi ya Yanga Princess. 


Yanga Princess kesho itakuwa ugenini Uwanja wa Simba Mo Arena kusaka pointi tatu ndani ya Ligi Kuu ya Wanawake ambayo imeanza kuwa na ushindani mkubwa.


Mgosi amesema:”Maandalizi yapo sawa na tunahitaji ushindi ili kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea ya kutwaa ubingwa Kwenye  hii ligi ya Wanawake.


“Tunaamini mchezo utakuwa mgumu ila tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na tunatambua kwamba kwa kiasi fulani Yanga imeanza kuimarika tofauti na ile ya msimu uliopita.


“Yote kwa yote wachezaji wetu wana morali kubwa na nimewaambia kwamba tunahitaji ushindi katika mchezo huo wa kesho ninaamini itakuwa hivyo,”.


Mazoezi ya Simba Queens yanafanyika Kwenye Uwanja wa Toto Tundu uliopo Tabata Segera ambapo ipo kambi ya timu hiyo kwa sasa ambao ni mabingwa watetezi.

MUANGOLA WA YANGA HATIHATI KUKOSA MECHI ZOTE ZA MZUNGUKO WA KWANZA MNIGERIA MIDO MAMBO SAFI YANGA,MABAO YA CHAMA NA SIRI YAKE,NDANI YA CHAMPIONI IJUMAA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply