Uncategorized

BOSI WA ZAMANI WA ASTON VILLA NA LIVERPOOL HOULLIER AFARIKI

admin December 14, 2020 3:47 pm

 


GERARD Houllier, aliyekuwa kocha wa zamani wa Klabu ya Liverpool ametangulia mbele za haki akiwa na umri wa miaka 73 na ujumbe wake wa mwisho alisema kuwa atapambana kurejea katika hali ya kawaida.

Houllier ambaye pia amewahi kuifundisha Klabu ya PSG, Aston Villa na Lyon alifanyiwa upasuaji hivi karibuni.

Amekuwa kwenye stori ndefu juu ya matibabu yake kwa kuwa alikuwa akitumia dawa na inatajwa kwamba tatizo la presha limesababisha kifo chake.

Alikiongoza kikosi cha Liverpool msimu wa 2001 ametajwa na wachezaji wa zamani kwamba ni miongoni mwa makocha bora wenye uwezo wa kufundisha kwa umakini.

Raia huyo wa Ufarasa ametangazwa pia kupitia vituo vya radio nchini humo ambapo kupitia RMC na magazeti ya Habari za Michezo L’Equire zimeripoti kwamba kocha huyo amefariki baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo Paris.

Kupitia kwa Vincent Duluc,aliripoti kwamba Houllier alifanyiwa upasuaji wiki tatu zilizopita na alirejea nyumbani Jumapili. 


Ameripoti ujumbe uliotumwa uliandikwa:”Ninapambana kwa sasa lakini ninadhani nitatoka katika hili,”.

AZAM FC YAINGIA ANGA ZA NYOTA ANAYEPIGIWA HESABU NA YANGA AZAM FC YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA NAMUNGO FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply