Uncategorized

KMC WATOA TAMKO KUHUSU PENALTI YA SIMBA KWA MKAPA

admin December 17, 2020 4:47 am

 


UONGOZI wa KMC umesema kuwa maamuzi ya penalti iliyotolewa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara jana, Desemba 16 hayapo mikononi mwao kwa kuwa hiyo sio kazi yao.

Wakati ikiyeyusha pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba, bao hilo lilipatikana kwa mkwaju wa penalti dakika ya 73 baada ya mwamuzi wa kati Elly Sassi kutafsiri kwamba mchezaji wa KMC aliunawa mpira huo.

Bao la ushindi lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 77 na na kuifanya timu hiyo kufikisha jumla ya poiinti 35 ikiwa nafasi ya pili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Habib Kondo, Kocha Msaidizi wa KMC amesema:” Kuhusu maamuzi ndani ya uwanja hilo benchi la ufundi hatujui, sisi kazi yetu ni kufundisha timu ili ipate matokeo na ndicho ambacho tunakifanya wakati wote.

“Ninachokijua mimi ni kwamba wachezaji wetu walipambana katika kusaka matokeo na tumepoteza hakuna cha kubadilisha zaidi ya mipango kwenye mechi zetu zijazo,”.

Tukio hilo  lilichukua dakika nne kwa wachezaji wa KMC kuwa kwenye ubishani na mwamuzi kwa kuwa hawakukubaliana na kitendo hicho .
JOSE MOURINHO:USHINDI WA LIVERPOOL NI WA KUTENGENEZWA KOCHA YANGA AFUNGUKIA KUHUSU USAJILI WAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply