Uncategorized

SIMBA WAANZA KUIVUTIA KASI FC PLATINUM

admin December 19, 2020 3:47 pm


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo Desemba 19 kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidiya FC Platinum.


Simba itakuwa na kazi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa nchini Zimbabawe.


Mchezo huo utachezwa Jumatano ya wiki ijayo, Desemba 23 ambapo utakuwa ni wa raundi ya kwanza na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Dar, Januari 6.

Vandenbroeck amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila watapambana kusaka matokeo chanya kwenye mchezo huo.


Kikosi kilikwea pipa jana Desemba 18 na msafara wa wachezaji 24.

YANGA WAENDELEZA REKODI YAO, WAPINDUA MEZA KIBABE MBELE YA DODOMA JIJI MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI SPOTI LA XTRA JUMAPILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply