Uncategorized

BAADA YA KUTEMBEZA KICHAPO CHA MABAO 7-0, LIVERPOOL NAFASI YA KWANZA MPAKA CHRISTMAS

admin December 20, 2020 10:47 am


USHINDI walioupata Liverpool wa mabao 7-0 dhidi ya Crystal Palace unawafanya wawe na uhakika wa kukaa nafasi ya kwanza mpaka Christmas kwa kuwa hakuna timu itakayowafikia kwa pointi.

Licha ya ushindi huo mkubwa ndani ya Uwanja wa Selhurst, Kocha Mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa bado hajafikia malengo yake.

Mohamed Salah dakika ya 81 na 84 na Roberto Firmino dakika ya 44 na 68 walitupia mabao mawilimawili, Jordan Henderson dakika ya 52, Sadio Mane dakika ya 35 na Takumi Minamino dakika ya 3 walitupia bao mojamoja.

Huu unakuwa ni ushindi mkubwa kwa Liverpool kwa msimu huu na wanajikita moja kwa moja nafasi ya kwanza mpaka Christmas itakapokamilika ili wampate atakayewarithi nafasi hiyo kwa kuwa kwa mechi zilizobaki hakuna ambaye anaweza kumshusha.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 14, imekusanya jumla ya pointi 31 na inafuatiwa na Everton yenye pointi 26 nayo pia imecheza mechi 14 huku Tottenham ikiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 13 ina pointi 25.

Rekodi hiyo inamfanya Klopp kushinda mechi nyingi ndani ya Ligi Kuu England kwa makocha wale ambao wamewahi kuifundisha timu hiyo.


Klopp amesema :-“Ulikuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa na kiukweli bado tuna kazi ya kufanya ili kuweza kufikia malengo kwani nia yetu bado haijaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa na tunatakiwa kuongeza juhudi.

“Nimefurahia ushindi na kupata pointi tatu nawapongeza wachezaji wamefanya kazi kubwa na ngumu katika kutafuta mafanikio,” .


FC PLATINUM YAPANGA MIKAKATI KUWAONDOSHA SIMBA RATIBA YA YANGA KUIVAA IHEFU YAPANGULIWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply