Uncategorized

NTIBANZOKIZA AWEKA REKODI YAKE BONGO

admin December 20, 2020 4:47 am


 NYOTA mpya wa Yanga, 
Saido Ntibazonkiza ameweka rekodi yakee ndani ya ardhi ya Bongo baada ya kufunga jumla ya mabao mawili na pasi moja kwenye mechi zake mbili za mwanzo. 

Ingizo hilo jipya kwenye usajili wa dirisha dogo kutoka nchini Burundi alianza kufanya makeke kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Singida United.

Mchezo huu ulikuwa ni wa kirafiki na matokeo ilikuwa Yanga 3-0 Singida United, Uwanja wa Liti ambapo alifunga mabao mawili, moja kwa penalti.


Jana Desemba 19 kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na matokeo yakuwa Yanga 3-1 Dodoma Jiji alitupia bao moja kwa faulo na pasi moja ambayo alipiga pia kwa njia ya faulo.


Rekodi yake imekuwa ya kipekee ndani ya ardhi ya Bongo kwa msimu huu kwa wachezaji ambao wamesajiliwa dirisha dogo kwa kuwa wengi hawajaanza kuonyesha makeke ikiwa ni pamoja na Thaddeo Lwanga wa Simba ambaye anatarajiwa kuanza kufanya yake Desemba 23.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI SPOTI LA XTRA JUMAPILI MIKAKATI YA AZAM FC KWENYE USAJILI YAWEKWA WAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply