Uncategorized

BEKI KISIKI WA YANGA MALI YA POLISI TANZANIA

admin December 24, 2020 8:47 am


 IMEELEZWA kuwa beki kisiki wa zamani wa Klabu ya Yanga, Kelvin Yondani amejiunga na Klabu ya Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu Malale Hamsini.


Yondani anajiunga na Polisi Tanzania akiwa ni mchezaji huru baada ya dili lake ndani ya Yanga msimu uliopita wa 2019/20 kukamilika na mabosi hao kushindwa kumuongezea mkataba mpya.


Awali ilielezwa kuwa nyota huyo amejiunga na Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morroco.


Habari kutoka ndani ya Polisi Tanzania zimeeleza kuwa nyota huyo amesaini dili miezi sita kinachosubiriwa ni utambulisho.


“Kweli Yondani anatakiwa na Polisi Tanzania, kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili na dili lake ni la miezi sita,” ilieleza taarifa hiyo.

AZAM YAMFUATA MRITHI HUYU WA DAVID KISSU MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply