Uncategorized

MRISHO NGASA KUIBUKIA GWAMBINA FC

admin December 24, 2020 10:47 am


 MRISHO Ngasa , kiungo wa zamani wa Klabu ya Yanga anatajwa kumalizana na mabosi wa Klabu ya Gwambina FC ambayo inamiliki Uwanja wa Gwambina Complex.

Ngasa mwenye uzoefu ndani ya Ligi Kuu Bara amecheza timu kubwa ndani ya ardhi ya Bongo ikiwa ni pamoja na Azam FC, Mbeya City na Simba kwa nyakati tofauti.


Pia aliweza kucheza ndani ya Klabu ya Ndanda FC ambao wamekuwa wakiweka wazi kwamba bado Ngasa ni mali yao kwa kuwa alipoachwa na Yanga  msimu wa 2019/20 alisani mkataba mpya huko kwa Wanandanda Kuchele.


Habari zimeeleza kuwa nyota huyo amesaini dili la mwaka mmoja kuungana na Mwinyi Zahera ambaye yupo kwenye benchi la ufundi akiwa ni Mkurugenzi.

“Kuhusu Ngasa kuna mambo ambayo yanakamilishwa hivyo ikiwa kila kitu kitakuwa sawa tutatangaza na taarifa itatolewa,” ilieleza taarifa hiyo.


Alipotafutwa Ngasa ili aweke wazi kuhusu ishu ya kuibukia Gwambina hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

MGOMBEA SIMBA APEWA MILIONI AZAM FC YAKUBALI MAMBO NI MAGUMU NDANI YA LIGI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply