Uncategorized

SIMBA NDANI YA BANDARI SALAMA

admin December 25, 2020 3:47 pm

 


KIKOSI cha Simba kimewasili salama ardhi ya Bandari Salama, Dar leo Desemba 25 kutoka nchini Zimbabwe.


Desemba 23 kilikuwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe kikisaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.


Kwenye mchezo huo kikosi hicho kilipoteza kwa kufungwa bao 1-0. Bao hilo la ushindi kwa FC Platinum ya nchini Zimbabwe lilipachikwa kimiani na Perfect Chikwende dakika ya 17.


Kimerejea kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya kuanza mbio za kutetea taji la Kombe la Shirikisho ambapo Jumapili, Desemba 27 kitamenyana na Majimaji ya Songea.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa na mshindi atasonga hatua inayofuata atakayepoteza safari itaishia Uwanja wa Mkapa.

BIASHARA UNITED HESABU ZAO ZA USAJILI NI KWA WASHAMBULIAJI EMMANUEL OKWI AMETIMIZA MIAKA 28

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply