Uncategorized

MTIBWA SUGAR YATUMA UJUMBE KWA RUVU SHOOTING

admin December 30, 2020 9:47 am


 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambao utakuwa ni wa zmunguko wa pili.

Mchezo wa kwanza kwa msimu wa 2020/21 timu hizi zilitoshana nguvu ya bila kufungana na waligawana pointi mojamoja.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

“Tuna mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa ila sisi tupo tayari na tunahitaji kupata pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

“Mchezo wetu wa kwanza tulitoshana nao nguvu na inatufanya tuzidi kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu ujao, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.

Utakuwa ni mchezo wa kwanza ndani ya 2021 kwa timu hizi mbili kukutana ndani ya uwanja. Utachezwa Januari 2,2021.

ARTETA AGOMA KUBADILI MPANGO WAKE KWENYE USAJILI MBELGIJI SIMBA AKWAA KIZINGITI CHA KUFUNGIA MWAKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply