Uncategorized

MANCHESTER CITY YATENGA KITITA CHA MAANA KUIPATA SAINI YA KANE

admin January 3, 2021 4:47 am


 KLABU ya Manchester City inataka kufanya mpango wa kutenga pauni 90m (Sh bilioni 281) kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane.

 

Kocha wa Man City, Pep Guardiola anataka kufanya hivyo ili kufanikisha mtu sahihi wa kuziba pengo la Sergio Aguero ambaye anasumbuliwa na majeraha.

 

Kane amekuwa mmoja wa washambuliaji wenye ubora wa juu kwa msimu kadhaa sasa, amekuwa akifunga mabao 20 au zaidi katika michuano yote kwa misimu sita iliyopita na ameshinda Tuzo ya Ufungaji Bora wa Premier League, mara mbili.

 

Kane amekuwa na nguvu kubwa pia katika timu ya taifa ya England na hata ngazi ya klabu akiwa na uwezo wa kufunga na kutoa asisti.

 

Ushirikiano wake na Son Heungmin umeifanya Tottenham kuwa na msimu mzuri.Upande wa Aguero, ameshafunga mabao 256 katika mechi 378 alichoichezea timu hiyo.

 

Akiwa na umri wa miaka 32, kwa sasa, Aguero hajapata nafasi ya kucheza mechi nyingi kutokana na majeraha kumuandama.

POCHETTINO ACHEKELEA KUPATA KAZI YANGA NA SIMBA ZAPIGANA VIKUMBO KUPATA SAINI YA BEKI HUYU WA KUSHOTO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply