Uncategorized

OLE GUNNER SOLSKJAER AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE

admin January 13, 2021 6:47 am

 


OLE Gunner Solskjaer,  Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa vijana wake wana akili na juhudi kubwa ndani ya uwanja jambo ambalo linampa furaha.


Kocha huyo ameongeza kuwa ushindi ambao wameupata mbele ya wapinzani wao unawapa nguvu ya kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo na anaamini watakuwa vizuri.

Manchester United ilishinda bao 1-0 dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Turf Moor na kuwafanya waongoze ndani ya Ligi Kuu England wakiwa na pointi 36 wakiwashusha mabingwa watetezi, Liverpool wenye pointi 33.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Paul Pogba dakika ya 71 ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo.

Ole amesema:”Vijana wamefanya kazi nzuri na kwa juhudi kubwa, hapo walipo wanastahili pongezi kwani sikutarajia kuona uwezo huo, imani yangu ni kwamba wataendelea kuwa bora muda wote ndani ya uwanja,” .

ISHU YA CHAMA NA LUIS KUIVAA YANGA LEO MAPINDUZI IPO HIVI HUYU HAPA ATAJWA KUWA MRITHI WA DAVID KISSU AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply