Uncategorized

SHEFFIELD YAPATAUSHINDIWA KWANZA PREMIER

admin January 14, 2021 8:47 am

 


TIMU ya Sheffield United, juzi ilifanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu England baada ya kuwachapa Newcastle United bao 1-0.

 

Katika michezo yake 17 iliyopita, vijana hao walifanikiwa kupata sare kwenye michezo miwili, wakipoteza michezo 15 kabla ya ushindi katika mchezo wa 18 Katika michezo yote hiyo, walikuwa wamefunga mabao nane tu na hili la juzi la tisa na kufungwa mabao 29.

 

Bao la pekee kwenye mchezo huo lilifungwa na Billy Sharp kwa mkwaju wa penalti jambo ambalo liliwafanya washangilie sana mwishoni mwa mchezo huo.

 

Wachezaji wa timu hiyo walionekana wakishangilia kama vile wametwaa ubingwa na hata kwenye vyumba waliendelea kushangilia kuonesha kuwa ni ushindi ambao wameusubiri kwa muda mrefu

TUISAPOTI TAIFA STARS IFANYE VIZURI CHAN KAZE AMKINGIA KIFUA MICHAEL SARPONG

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply