Simba SC

CHIKWENDE ATAJA KITAKACHOMBEBA SIMBA

admin January 20, 2021 2:47 pm

KIUNGO mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba, Tatenda Perfect Chikwende amesema anaamini uwepo wa mashindano mengi ambayo Simba inashiriki ni miongoni mwa vitu vitakavyomsaidia kukuza kiwango chake.

Chinkwende amejiunga na Simba akitokea kwenye kikosi cha klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe baada ya kuonyesha uwezo kwenye michezo miwili aliyocheza dhidi ya Simba.

Simba iliiondosha FC Platinum kwa jumla ya mabao 4-1 na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika huku huku bao pekee la Platinum likifungwa na Chikwende.

Akizungumzia maisha yake mapya ndani ya Simba Chikwende amesema: “Nipo tayari kutumika kuisaidia Simba, nafurahi kuwepo hapa na najua nitapata nafasi kubwa yakukuza kiwango changu maradufu kutokana na ukweli kwamba Simba inashiriki michuano mingi hivyo ni nafasi kwangu kucheza mara kwa mara,”

WINGA MKONGO AFUNGUKIA DILI LAKE SIMBA KAZE ANOGESHA SHANGWE LA UBINGWA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply